Pata taarifa kuu
FRANCE 24-RFI

France 24 Kiingereza yaanza kuonekana Kenya bila malipo

France 24 imekuwa Televisheni ya kwanza ya Kimataifa kuzindua matangazo yake kwa lugha ya Kiingereza kuonekana bila malipo nchini Kenya kupitia kinga’muzi kinachomilikiwa na Serikali Signet.

Marc Saikali Mkurugenzi wa France 24 akihojiwa na mwanahabari wa RFI Kiswahili Victor Abuso. 28 Machi 2018.
Marc Saikali Mkurugenzi wa France 24 akihojiwa na mwanahabari wa RFI Kiswahili Victor Abuso. 28 Machi 2018. RFI Kiswahili
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa France 24 Marc Saikali amesema uwepo wa Televisheni hiyo inayoonekana katika miji 20 nchini humo, inawezesha watazamaji kupata ladha mpya ya Habari za Kimataifa.

Aidha, amesema watazamaji sasa watapata fursa ya kuunganishwa na maeneo mengine ya dunia kupitia France 24 lakini pia kinachotokea nchini Kenya kitafahamika duniani.

“Tumekuja Kenya, kuwapa watazamaji mtazamo mpya wa Habari za Kimataifa na kuwaelewesha kwa lugha rahisi kuhusu kinachotokea duniani,”. alisema Saikali.

“Lengo la France 24 sio kuleta ushindani, kujitangaza au kufanya biashara ,” aliongeza.

Pamoja na hayo, Saikali amesema sera ya Televisheni hiyo ni kutangaza ukweli wa matukio yanayoendelea duniani, ili watazamaji wawe na uelewa na kuifahamu vema duniani ilivyo

Jean-Marc Belchi Mkurugenzi wa Maendeleo ya France Media Monde barani Afrika amesema kuzinduliwa kwa matangazo hayo ya Kiingereza bila malipo kutaongeza watazamaji barani Afrika kufikia Milioni zaidi ya 50 katika mataIfa zaidi ya 100.

Nchini Kenya pekee, watazamaji wa France 24 wanatarajiwa kuongezeka kutoka Milioni moja hadi Milioni Mbili.

Hatua hii imewafurahisha baadhi ya Wakenya ambao wamesema mambo yanayoendelea katika nchi yao. yatapata mtazamo mpya duniani.

“Kuwepo kwa France 24 hapa Kenya kuonesha ushirikiano wa karibu kati ya Kenya na Ulaya na itaisaidia nchi yetu kunufaika kibiashara,” amesema Wachera Ngunjiri.

Uongozi wa France 24 unasema, uwepo wake nchini Kenya sio kwa manufaa ya kisiasa bali ni kuleta Habari za dunia kwa mtazamo na ladhaa tofauti kwa raia wa nchi hiyo.

Wakenya sasa wameanza kutazama France24 kwa lugha ya Kiingereza bila malipo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.