Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Ansbert Ngurumo :Wanahabari wa Tanzania msikate tamaa

media Magazeti nchini Tanzania wikipedia

Mwandishi wa habari mkongwe wa Tanzania, Ansbert Ngurumo aliyekimbilia uhamishoni nchini Finland kwa madai ya kutishiwa maisha na maofisa wa serikali amewataka waandishi wa habari na wanaharakati nchini humo kutorudi nyuma katika kupigania uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu.

Mwandishi huyo amesambaza andiko kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii akieleza kuwa amelazimika kuondoka nchini Tanzania kutokana na kuwepo kwa mipango ya kuangamiza maisha yake. Kwa sasa anaishi nchini Finland alikopata hifadhi.

Akizungumza katika mahojiano na RFI Kiswahili kutoka nchini Finland, Ngurumo ambaye alipata kuandikia na kuwa mhariri wa magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi amekiri licha ya kutokuwepo Tanzania ataendelea kuandika mambo yanayohusu nchi hiyo.

“Ingawa sipo huko, najua kinachoendelea Tanzania na nitaendelea kuandika kuhusu nchi yangu, kinachonifanya niwe hapa (Finland), nataka kuwa hai. Ninawaomba,”amefahamisha na kuwaasa waandishi wa habari kujihadhari.

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania, Ngurumo amesema haupo tena akitolea mfano wa habari zinazoandikwa na magazeti na zinazotangazwa na redio na luninga.

“Kuna masuala mengi ya msingi yanayopaswa kuhojiwa lakini yanafia chini kutokana na mazingira yalipo Tanzania. Woga umetawala katika vyombo vingi vya habari, wahariri na wamiliki.

RFI Kiswahili imemtafuta Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas ambaye alisema serikali ya Tanzania haina kauli juu ya suala hilo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana