Pata taarifa kuu
UN-BURUNDI-NKURUNZIZA

UN:Burundi haijaboresha haki za binadamu

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanywa na Serikali ya Burundi kuboresha na kulinda haki za binadamu.

Picha ya mwandamanaji jijini Bujumbura akiwa amefungwa wakati wa maandamano mwaka 2016
Picha ya mwandamanaji jijini Bujumbura akiwa amefungwa wakati wa maandamano mwaka 2016 REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama
Matangazo ya kibiashara

Tangu kuibuka kwa mzozo wa kisiasa nchini Burundi mwaka 2015 Umoja wa Mataifa umekuwa ukikosoa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi, vitendo vilivyosababisha maelfu ya raia kuikimbia nchi yao kuhofia kukamatwa, kuteswa na kuuawa.

Hivi sasa Tume hii inasema tangu kuchapisha ripoti yake kuhusu mwenendo wa haki za binadamu nchini Burundi, hakuna kilichobadilika nchini humo na vitendo hivyo vimeendelea kushuhudiwa.

Serikali ya Burundi imeendelea kukanusha ripoti za Umoja wa Mataifa, na kusema kuwa utafiti wake ni wa uongo na badala yake kusisitiza kuwa amani imerejea nchini humo.

Rais Pierre Nkurunziza amekuwa akiwataka wakimbizi wanaoishi nje ya nchi hiyo kurejea nyumbani, hatua ambayo wakimbizi hao wamekataa.

Mwezi Mei mwaka huu kutakuwa na kura ya maoni kuibadilisha katiba ya nchi hiyo ili kuibadilisha Katiba kumwezesha rais Nkurunziza kuongoza hadi mwaka 2034.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.