Pata taarifa kuu
KENYA-BUNGE-SIASA

Wabunge na Maseneta nchini Kenya waunga mkono mwafaka kati ya rais Kenyatta na Odinga

Wabunge na Maseneta wa serikali na upinzani nchini Kenya wamesifia mwafaka uliofikiwa kati ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga kukubaliana kujadili masuala mbalimbali yanayolikabili taifa hilo baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2017.

Bunge la Kenya
Bunge la Kenya www.voanews.com
Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi hao wamesema kilichokubaliwa kati ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa NASA Raila Odinga kilikuwa ni kitendo cha kishujaa ambacho kitaleta umoja wa kisiasa na maendeleo nchini humo.

Kiongozi wa wachache katika bunge la Senate Moses Wetangula, amesema kilichokubalika, kitekelezwa mara moja ili Kenya mpya ianze kuonekana baada ya kipindi kigumu cha kisiasa.

Aidha, amesema  mazungumzo hayo yatakuwa magumu, ambayo huenda kila mmoja hataridhika lakini kikubwa iwe ni kuleta amani na maendeleo nchini humo.

Naye kiongozi wa walio wengi Kipchumba Murkomen, amesema kilichokubaliwa na viongozi hao kimeanza kuponya tofauti za kisiasa nchini humo baada ya kipindi kigumu cha Uchaguzi.

Naye Seneta mkongwe Yusuf Haji amesema, Kenya imeanza kupumua hewa ya matumaini baada ya mkataba kati ya viongozi hao wawili.

Kiongozi wa walio wachache katika bunge la Kitaifa, John Mbandi amesema Kenya imeanza kwenda katika njia nzuri baada ya mkataba huo.

"Mwafaka huo sio kuunganisha upinzani na serikali  au kuunda serikali ya muungano bali ni kujadliana kuhusu hali ya  maendeleo na demokrasia nchini," alisema Mbandi.

"Tutaunga mkono juhudi za serikali kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo," aliongeza Mbandi.

Rais Kenyatta na Odinga walikubaliana kuunda Kamati ya pamoja kujadili masuala yanayolikabili taifa hilo hasa siasa za kikabila, malalamiko ya Uchaguzi, uwakilishi sawa, mfumo wa uongozi, uhuru wa Mahakama, ufisadi miongoni wa masuala mengine.

Viongozi hao walikubaliana kujadili na kutafutia suluhu changamoto hizi mwafaka kwa pamoja bila ya kuegemea upande wowote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.