Pata taarifa kuu
KENYA-ETHIOPIA-WAKIMBIZI

Kenya yapokea wakimbizi zaidi ya 5,000 kutoka Ethiopia

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya linasema raia wa Ethiopia wapatao 5,000 wamekimbilia nchini humo kuomba hifadhi tangu tarehe 10 mwezi Machi.

Wakimbizi wa Ethiopia waliokimbilia mjini Moyale katika mpaka na Kenya
Wakimbizi wa Ethiopia waliokimbilia mjini Moyale katika mpaka na Kenya www.kassfm.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Shirika hilo Abbas Gullet amesema wakimbizi zaidi wanatarajiwa kuwasili nchini humo hasa mjini Moyale katika mpaka wa nchi hizo mbili.

Raia hao wa Ethiopia wamekimbilia nchini Kenya baada ya jeshi kuanza kufanya oparesheni ya kuwatafuta makundi ya waasi wa kundi la Oromo Liberation Front.

Wakimbizi watano wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Rwanda baada ya wakimbizi kupigania chakula cha msaada.

Wiki iliyopita, jeshi la Ethiopia liliwauwa raia 9 wasiokuwa na hatia katika mpaka huo na Kenya katika harakati za kupambana na waasi. Jeshi limesema linachunguza tukiio hilo.

Mzozo wa kiusalama nchini humo umesababisha hali ya hatari kutangazwa kwa muda wa miezi sita nchini humo.

Watu wa jamii ya Oromo wameendelea kulalamika kuwa wametengwa kimaendeleo na serikali jijini Addis Ababa na kuamua kuandamana na kupambana na wanajeshi wa serikali.

Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn alijiuzulu mwezi uliopita na chama tawala na sasa kinatarajiwa kumtaja kiongozi mpya mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.