Pata taarifa kuu
RWANDA-RADI-MAAFA

Watu 16 waliouawa kwa kupigwa radi nchini Rwanda wazikwa

Watu 16 waliouawa Jumamosi iliyopita baada ya kupigwa radi wakiwa katika Kanisa la Waadventista Wasabato katika Wilaya ya Nyaruguru nchini Rwanda wamezikwa.

Mazishi ya watu 16 walipigwa na radi nchini Rwanda wakati wa ibada ya mazishi Machi 11 2018
Mazishi ya watu 16 walipigwa na radi nchini Rwanda wakati wa ibada ya mazishi Machi 11 2018 www.newtimes.co.rw
Matangazo ya kibiashara

Wauamini wote walizikwa katika Makaburi ya Nyabimata katika mazishi ambayo yalihudhuriwa na mamia ya waombolezaji.

Meya wa Wilaya ya Nyaruguru Habitegeko Francois ameliambia Shirika la Habari za Ufaransa AFP kuwa watu 14 walipoteza mara mmoja huku wengi wawili wakipoteza maisha wakiwa hospitalini.

Waumini wengine 140 walijeruhiwa baada ya kutokana na radi hiyo iliyoambatana na mvua kubwa na wanaendelea kupata matibabu katika hospitali mbalimbali katika Wilaya hiyo.

Mwanafunzi mmoja alipoteza maisha huku wengine 17 wakijeruhiwa katika tukio hilo baya ya kiasili kuwahi kutokea Rwanda katika siku za hivi karibuni.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.