Pata taarifa kuu
UFARANSA-TANZANIA-ELIMU

Ufaransa kuisaidia Tanzania katika Elimu ya Juu

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frédéric Clavier amesema serikali yake ipo tayari kuongea ushirikiano na serikali ya Tanzania katika elimu ya chuo kikuu ili kuongeza hamasa ya wanafunzi kusoma Sayansi

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier akiwa na Rais wa nchi hiyo Dokta John Pombe Magufuli hivi karibuni
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier akiwa na Rais wa nchi hiyo Dokta John Pombe Magufuli hivi karibuni twitter.com/FranceTanzania
Matangazo ya kibiashara

Clavier ameyasema hayo mara baada ya kuhitisha mkutano wa siku tatu wa wanawake na maendeleo endelevu barani Afrika uliojikita kuangalia umuhimu wa sayansi katika maendeleo ya wanawake barani humo.

“Kwa Serikali ya Ufaransa nina imani kwamba tupo tayari kusaidia maazimio mawili au matatu tuna mkakati ambao ni kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Ufaransa hasa katika mahusiano ya vyuo vikuu “alisema Clavier.

Akizungumzia Maazimio ya Mkutano huo, Rais wa Taasis ya Taaluma ya Sayansi nchini humo TAAS Profesa Esther Mwaikambo amesema mkutano huo uliojumuisha wanawake wabobevu katika Sayansi umeweka maazimio manne ili kuwasaidia wasichana kujikita katika Sayansi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kuhamasisha umuhimu wa wasichana kusoma masomo hayo.

“Mila na Desturi potofu zinachangia wasichana kutoona umuhimu wa kusoma masomo ya sayansi,tunaendelea kuwaeleza umuhimu ya kuziacha mila potofu ili wasichana wasome”alisema Profesa Mwaikambo.

Miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na Kuziomba serikali kuimarisha elimu ya Afya ya Uzazi kwa wanafunzi tangu wakiwa shule za Msingi ,Beng'i Issa ni katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Tanzania anasema serikali ya Tanzania inasisitiza umuhimu wa wasichana kusoma pamoja na kufundisha elimu ya afya ya uzazi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.