Pata taarifa kuu
EAC-EALA-SIASA-WANAWAKE

Jumuiya ya Afrika Mashariki yataka wanawake kushika nyadhifa zaidi za kisiasa

Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki inataka wanawake zaidi kujumuishwa katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ili kusaidia kufanikisha maendeleo ya Jumuiya hiyo inayowaleta pamoja nchi sita.

Baadhi ya viongozi wa wanawake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki katika moja ya mikutano yao
Baadhi ya viongozi wa wanawake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki katika moja ya mikutano yao www.eala.org
Matangazo ya kibiashara

Wakati siku hii ikitumiwa kukumbuka na kutambua mchango wa wananwake duniani, wanawake kutoka Afrika Mashariki wanataka haki zao kuheshimiwa na kuwa na usawa wa kijinsia katika nyadhifa za uongozi.

Mkataba uliounda Jumuiya ya Afrika Mashariki umetoa fursa kwa nchi wanachama kuhakikisha kuwa wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika maendeleo na mafanikio ya Jumuiya hiyo.

Katiba za mataifa yote ya Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini inaeleza kuwa, moja ya tatu ya nyadhifa zote za uongozi, ni lazima zishikiliwe na wanawake.

Rwanda inaongoza katika uwakilishi wa wanawake bungeni kwa asilimia 63.8 , ikifuatwa na Burundi ambayo wabunge wanawake ni asilimia 36.4.

Tanzania inawasilishwa na asilimia 36, Uganda 35 huku Kenya ikiwa ya mwisho kwa asilimia 20 ya wanawake bungeni.

Malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuwa na uwakilishi wa asilimia 50 kwa 50 wa jinsia katika nyanja zote za uwakilishi ikiwa ni pamoja na siasa, elimu, ajira na nyadhifa nyingine kufikia mwaka 2030.

Margaret Zziwa kutoka Uganda anaingia katika vitabu vya historia kuwa mwanamke pekee na wa kwanza kuwa spika wa bunge la Afrika Mashariki EALA tangu kuanza kazi yake mwaka 2001.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.