Pata taarifa kuu
KENYA-UFISADI-UHURU KENYATTA

Serikali ya Kenya haiwezi kueleza ilivyotumia Dola Milioni 400

Serikali ya Kenya haiwezi kueleza matumizi ya fedha za umma Dola za Marekani Milioni 400, kwa mujibu wa ripoti ya mkaguzi wa serikali Edward Ouko.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta .
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta . REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii inaonesha namna maafisa wa serikali ya rais Uhuru Kenyatta walivyoshindwa kuelekeza matumizi ya fedha katika mwaka wa fedha wa 2015/2016.

Hata hivyo, ripoti hiyo imeeleza kuwa ni thuluthi tatu ya idara za serikali ndizo zilizoweza kueleza kikamilifu matumizi ya fedha za umma ilizotengewa kwa miradi mbalimbali.

Wizara ya Ulinzi imeshtumiwa kwa kununua ndege ya kijeshi kwa kutumia Milioni 15 mwaka 2007, lakini ndege hiyo haijawahi kutumiwa na sasa inatumiwa kama eneo la kuchukua vifaa vya kubadilishia ndege zinazoharibika.

Aidha, Wizara ya Mambo ya ndani inayohusika na usalama, imeshindwa kuelekeza namna ilivyotumia Dola Milioni 1.7 kununua viatu vya askari 51,500.

Kenya imeendelea kukabiliwa na visa vya ufisadi huku serikali ikishtumiwa kushindwa kuwaajibisha wala rushwa.

Shirika la Kimataifa la kupambana na ufisadi la Transparency International linaorodhesha Kenya katika nafasi ya 143 kati ya 180 katika vita dhidi ya ufisadi.

Rais Uhuru Kenyatta amewahi kunukuliwa akisema kuwa hana mamlaka ya kuamuru washukiwa kufunguliwa mashtaka kwa sababu ni kazi ya Tume ya kupambana na ufisadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.