Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Kim Jong-un ataka mkutano wa pili na Donald Trump "kwa tarehe ilio karibu" (Moon Jae-in)
E.A.C

Hali ya tahadhari nchini Kenya baada ya maambukizi ya homa hatari

media Vipimo vya homa ya H1N1 influenza.

Maafisa wa afya nchini Kenya wametangaza hali ya tahadhari baada ya watu 15 kulazwa Hospitalini katika Kaunti ya Laikipia baada ya kuambukizwa homa hatari inayohamika kwa jina la H1N1 influenza.

Mkurugenzi Mkuu wa afya katika Kaunti hiyo Donald Mogoi amesema mtoto wa miaka mitano alifariki dunia wiki mbili zilizopita kutokana na homa hiyo.

Watu 60 waliokuwa na wasiwasi wa kuambukizwa homa hiyo, walikwenda kupimwa na 15 kulazwa hospitalini.

Dalili za homa hiyo hatari ni pamoja na kupanda kwa joto, kuharisha, kutapika, kuwa na kikohozi kikavu na kukosa nguvu.

Madaktari wanaonya kuwa, homa hii huwaathiri sana watoto wachanga na inaweza kusambazwa kupitia njia ya hewa.

Kuepuka kuambukizwa, mtu anastahili kuepuka kugusana na mtu aliyeathiriwa lakini pia kuepuka kukusanyika katika eneo ambalo kumeripotiwa kutokea kwa homa hiyo.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana