Pata taarifa kuu
KENYA-MADAKTARI-HOSPITALI

Madaktari wanaopata mafunzo Hospitali ya taifa ya Kenyatta wagoma

Madaktari wanaopata mafunzo ya juu wakiwa kazini katika Hospitali ya taifa ya Kenyatta nchini Kenya, wamegoma baada ya kusimamishwa kazi kwa mwenzao baada ya kutokea kwa hitilafu ya upasuaji wa mgonjwa katika hospitali hiyo kubwa ya rufaa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Madakatri katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya
Madakatri katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya http://knh.or.ke/
Matangazo ya kibiashara

Madaktari hao wapatao 700 wamesema hawatarudi kazini hadi pale uongozi wa Hospitali hiyo iliyo jijini Nairobi,  itakapotatua changamoto zinazojiri kwa sasa na mwenzao kurejeshwa kazini.

Imeripotiwa kuwa mgonjwa huyo alifanyiwa upasuaji kichwani kimamosa , hatua ambayo imeikasirisha Wizara ya afya nchini humo na kuamua kumsimisha kazi Daktari, Manesi na wasaidizi wengine waliokuwa wanamhudumia mgonjwa huyo.

Aidha, kumekuwa na ripoti kuwa mgonjwa huyo alifariki dunia lakini, uongozi wa Hospitali hiyo umekanusha na kusema mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji anaendelea kupata matibabu.

Waziri wa afya Sicily Kariuki amempa likizo ya lazima Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Bi. Lily Koros na Mkurugenzi wa Wauguzi Bernard Githae.

Haya yanajiri, mwezi mmoja tu baada ya kuripotiwa kwa visa vya wanawake wanaojifungua kubakwa na wahudumu wa kiume katika hospitali hiyo usiku wanapokwenda kuwanyonyesha wanao lakini pia baada ya mwanamke mmoja kumwiba mtoto mchanga kabla ya kupatikana.

Hospitali hiyo inategemewa na Wakenya wenye kipacho cha chini wakiwemo watu wengine kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutokana na kutoa huduma kwa bei nafuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.