Pata taarifa kuu
KENYA-NJAA-USALAMA

Kenya yaanza kuwahudumia raia wanaokabiliwa na baa la njaa

erikali ya Kenya imeanza kusambaza msaada wa chakula kwa wakazi wa kaskazini mwa ukanda pwani ambao wameathirika na baa la njaa kutokana na ukame  unaoshudiwa, ambao pia umechangia uhaba mkubwa wa maji safi kwa matumizi wa binadam.

Bwawa la Barikiwa, halina maji kwa miezi 7 sasa, lilikua likisaidia karibu watu 300 (Bamba, Kaunti ya Kilifi).
Bwawa la Barikiwa, halina maji kwa miezi 7 sasa, lilikua likisaidia karibu watu 300 (Bamba, Kaunti ya Kilifi). RFI/Laure Broulard
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mshikamano nchini Kenya Eugine Wamalwa akihojiwa na mwandishi wa RFI-Kiswahili Joseph Jira, ameasema tofauti na maeneo mengi ya nchi ambayo yameathirika na baa la njaa, serikali pia inapanga kusambaza chakula cha msaada katika maeneo hayo ili kunusuru maisha ya Wakenya wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

"Zile kaunti zimeathirika hapa ni Tanariver, ukienda upande wa Kilifi pahala kama Bamba kuna shida ya uhaba wa chakula, hata Taita Taveta. Tayari malori ya vyakula yanaelekea kule, na tutahakikisha hakuna Mkenya anafariki kutokana na baa la njaa"

Waziri Wamalwa ameongeza kuwa serikali inafahamu athari za ukame maeneo yalioathirika, na wameweka malori ambayo yatakuwa yakisambaza maji ili kunusuru maisha ya mifugo pamoja na wananchi.

"Tumepokea zaidi ya magunia elfu 90, katika maghala ya nafaka nchini. Tuko na zaidi ya magunia milioni 3, kwa hivyo hatutaki Wakenya wawe na hofu, na sio kwamba eti tutapeleka chakula peke yake lakini pia tuhakikishe kuna maji."

Wakazi wa eneo la Kilifi kaskazini walioathirika na ukame, wameelezea masikitiko yao kufuatia hali hiyo inayowakumba, huku wengine wakiomba msaada zaidi.

"Mvua ya mwisho ilinyesha mwezi Novemba mwaka jana, na ilinyesha tu masaa kadhaa, ” mmoja wa wakazi wa Kilifi amesema.

Owen Baya mbunge wa Kilifi Kusini, amesema madeni ambayo serikali za kaunti zimekuwa zikidaiwa na kampuni ya kusambaza maji ukanda wa pwani pia yamechangia wananchi kuathairika zaidi.

"Hili deni limedumu kwa muda mrefu, na hili deni lilianza kabla ya serikali za ugatuzi ama kaunti kuanza, hivyo basi kuambia serikali za kaunti walipe deni hili, ni kuwaambia wachukue madeni ambayo hayakuwa, " amesema mbunge wa Kilifi, Owen Baya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.