Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Waziri wa Michezo wa Ufaransa azuru Rwanda

media Laura Flessel, Waziri wa Michezo wa Ufaransa. RFI/ Pierre René-Worms

Waziri wa michezo wa ufaransa Bi. Laura Flessel amefanya ziara ya siku tatu wakati ambapo uhusiano baina ya mataifa Ufaransa na Rwanda ukiwa hauko imara.

Wakiongea na wanahabari, waziri wa michezo na utamaduni wa Rwanda Bi Uwacu Jullian amekanusha madai kwamba, uhusiano baina ya mataifa hayo mawili hauko sawa.

Ziara hiyo imeanzia katika eneo la kumbukumbu la mauaji ya kimbali lililopo gisozi jijini hapa na waziri huyo wa michezo wa ufaransa Bi. Laura Flessel ameonesha heshima kubwa kwa kuinamia miili laki mbili na elfu hamsini iliyohifadhiwa katika eneo hilo kisha akaelekea katika wizara ya michezo na utamaduni iliyopo Remela jijinni Kigali ambapo amekutana na mwezake wa Rwanda na kufanya mazungumzo.

Wakiongea na waandishi wa habari muda mfupi mara baada ya kufanya mazungumzo ya faragha, waziri wa michezo wa Ufaransa amesema, uhusiano baina ya mataifa haya mawili unaweza kuwa imara zaidi hasa kupitia michezo.

"Leo hii kupitia michezo tunaweza kuzungumzia amani na kutafakari mustakabari wa maisha ya kizazi kijacho, twaweza pia kuzungumzia elimu pamoja na kupambana na viashiria vyote ambavyo vinaweza kuwashawishi vijana wetu kufanya maandamano, kupitia michezo tunaweza kufanya mengi, iwe katika Nyanja ya Elimu, afya, uchumi na hata siasa, uwepo wangu hapa kama waziri, mwanamichezo na mwanamke pia, faraja kubwa kwangu, “ amesema Waziri Laura Flessel .

Hii ni ziara ya kwanza ambayo imefanywa na waziri anayehudumu katika serikali ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron imekuja ikifuata ziara ya rais mstaafu wa Ufaransa Nicolaus Sarkozy mapema mwaka huu.

Ziara hizo zimefanywa wakati uhusiano baina ya mataifa haya mawili ukiwa mbovu madai ambayo hata hivyo yamekanushwa vikali na waziri wa michezo na utamaduni wa Rwanda, Bi. Uwacu Julienne.

“Uhusiano baina ya Rwanda na Ufaransa si mbaya kwani tuna balozi na chi zote zinawakilishwa, Wanyarwanda wanaenda ufaransa vivo hivyo wafaransa huja nchini Rwanda, japo kuna mambo ambayo hayako sawa lakini haimaanishi kwamba uhusiano baina ya mataifa haya ni mbaya, “ Bi. Uwacu Julienne .

Ikumbukwe uhusiano wa ufaransa na Rwanda ulianza kuyumba pale majaji wa Ufaransa walipotoa waranti ya kuwakamata maofisa wa juu wa jeshi la Rwanda RDF kwa madai kwamba, ndiyo waliohusika kwa namna moja ama nyingine na utunguaji wa ndege ya aliyekuwa rais wa Rwanda wakati huo Juvenal Habyarimana madai yanayokanushwa vikali na serikali ya Kigali.  

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana