Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini kumalizika Ijumaa

media Mgogoro unaosababishwa na machafuko ya kikabila umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na karibu watu milioni nne kuyatoroka makazi yao na kusababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu. REUTERS/David Lewis

Kikao cha mwisho cha mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yanayosimamiwa na Ethiopia kinaweza kumaliza leo Ijumaa kwa kufikia makubaliano ya kusitishwa kwa vita, mjumbe wa Umoja wa Mataifa David Shearer amesema.

Mazungumzo hayo, ambayo yalianza Februari 5 mjini Addis Ababa, yana lengo la kupata suluhisho la mojawapo ya migogoro mabaya zaidi barani Afrika.

"Tunatumaini kuwa kutakuwa na aina ya makubaliano yatakayosainiwa kesho (Ijumaa)," Shearer aliwaambia waandishi wa habari. "Inawezekana mkataba huo ukachelewa kuliko tulivyotarajia, lakini hali hiyo inaweza kutoa aina ya majadiliano."

Majadiliano nchini Ethiopia yalijikita kuhusu utawala na usalama.

Umoja wa Afrika na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametishia kuweka vikwazo dhidi ya wale wanakwamisha juhudi za amani nchini Sudan Kusini.

Sudan Kusini iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwezi Desemba 2013 wakati Rais Salva Kiir alimshtumu makamu wa rais wa zamani Riek Machar kupanga mapinduzi dhidi ya serikali.

Mgogoro unaosababishwa na machafuko ya kikabila umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na karibu watu milioni nne kuyatoroka makazi yao na kusababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana