Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA

Kura ya maoni Burundi: polisi yaonya wale wanatetea kura ya "hapana"

Polisi ya Burundi imewaonya vijana dhidi ya jaribio lolote la kuharibu usalama wa umma baada ya wanafunzi kadhaa na mwalimu mmoja kukamatwa katika mkoa wa Ngozi, mkoa anakotoka rais Pierre nkurunziza.

askari polisi wakipiga doria katika mtaa moja mjini Bujumbura, Burundi
askari polisi wakipiga doria katika mtaa moja mjini Bujumbura, Burundi REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Polisi ya Burundi imewaonya vijana dhidi ya jaribio lolote la kuharibu usalama wa umma baada ya wanafunzi kadhaa na mwalimu mmoja kukamatwa katika mkoa wa Ngozi, mkoa anakotoka rais Pierre nkurunziza.

Vijana hawa na mwalimu huyo walikua wakifanya kampeni wakiwahamasisha raia kupiga kura ya "hapana" wakati wa kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba inayopangwa kufanyika hivi karibuni. Marekebisho hayo yanakwenda kinyume na mkataba wa amani wa Burundi uliofikiwa mjini Arusha nchini Tanzania mnamo mwaka 2000. upinzani umeendelea kupinga marekebisho hayo ya katiba, ukibaini kwamba ni njama za rais Pierre Nkurunziza kutaka kusalia madarakani

Hivi karibuni Makamu wa rais wa Burundi Gaston Sindimwo alihakikisha kwamba pande zote mbili, "ndiyo" na "hapana" zinaweza kufanyiwa kampeni, huku akisema kuwa Tume ya Uchaguzi bado haijatangaza kuanza kwa kampeni hiyo. Upinzani na vyama vya kiraia wanashtumu marekebisho hayo ya katiba wakisema ni kampeni ya kumpigia debe rais Nkurunziza. Hayo yanajiri wakati ambapo kuna video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo afisa mmoja wa chama tawala anaonekana akisema anajiandaa "kuvunja meno ya wapinzani wa ndiyo". Video hiyo imezua hali ya sintofahamu.

Msemaji wa polisi, Pierre Nkurikiye amesema kuwa hata kama wanaharakati wa kura ya "hapana" wamekamatwa leo, maafisa wa polisi wanafanya kazi yao kwa mujibu wa sheria. "Onyo hilo limetolewa hasa kwa vijana, ambao wanadanganywa na baadhi ya wanasiasa. Mfano wa hivi karibuni ni wanafunzi ambao walikamatwa jana na leo [Jumanne] na mwalimu na wanafunzi wawili, ambao jana karibu saa 12 jioni walikua wakipita nyumba kwa nyumba kuhamasisha raia kupiga kura ya "hapana",PierreNkurukiye amesema .

"Vijana wanapaswa kutafakari historia ya nchi yetu. Hasa historia ya hivi karibuni. Na wakati huu, polisi wamepokea amri ilio wazi. Polisi imeombwa kufanya kazi kitaaluma na kutopuuzia jambo lolote na uimarishaji, kwa mujibu - bila shaka - wa sheria, "ameongeza Bw Nkurikiye.

Hayo yanajiri wakati ambapo Shirika la umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) linasema linahitaji milioni 391 mwaka huu 2018 ili kusaidia wakimbizi 430,000 wa Burundi katika nchi jirani za Tanzania, Rwanda, Uganda na DRC. UNHCR inasema inatarajia kuwapokea mwaka huu 2018 wakimbizi wapya 50,000 kutoka Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.