Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Vituo vya Citezen TV na Inooro TV vyafunguliwa Kenya

media Vituo vya runinga vya Citizen TV na Inooro Tv vimeruhusiwa kurusha matangazo yao nchini Kenya, wiki moja baada ya mitambo yao kuzimwa na serikali. twitter.com/citizentvkenya

Vituo vya runinga vya Citizen TV na Inooro Tv vimefunguliwa tena nchini Kenya baada ya kufungiwa kwa zaidi ya wiki moja.

Vituo hivi viwili ndivyo vilivyokuwa vimesalia kurejeshwa hewani, baada ya KTN News na NTV kufunguliwa mapema wiki hii.

Serikali ilizima mitambo ya runinga hizo wiki iliyopita, baada ya kudai kuwa vilikuwa vimepanga kuonesha moja kwa moja kuapishwa kwa kiogozi wa muungano wa upinzani NASA, kama rais wa wananchi.

Mashirika ya kiraia, yale ya kutetea haki za binadamu na raia wa Kenya wamelaani serikali kwa hatua hii, katika kile kinachoonekana kuwa, ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya Habari nchini Kenya.

Mahakama Kuu jijini Nairobi, iliagiza serikali kuwasha mitambo ya Televisheni tatu zilizozuiwa baada ya kudaiwa  kuwa na mpango wa kupeperusha moja kwa moja zoezi la kuapishwa kwa kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, kuwa rais wa watu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana