Pata taarifa kuu
BURUND-RADIO-UN

Burundi: UN yafadhili kituo cha radio cha taasisi ya mke wa rais.

Mkanganyiko umeibuka nchin Burundi kufuatia Umoja wa Mataifa kufadhili radio inayomilikiwa na taasisi ya fondation Ubuntu inayomilikiwa na mke wa rais wa Burundi Denis Nkurunziza na ambayo inapeperusha matangazo yake kutoka Mkoani Buye kaskazini mwa Burundi ambapo baadhi wanajiuliza iwpao ni jukumu la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (Kushoto) na mkewe Denis Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (Kushoto) na mkewe Denis Nkurunziza wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Ni msaada ambao umezua maswali, unaoundwa na vifaa vya studio ya radio ya taasisi ya mke wa rais wa Burundi na ambao thamani yake inakadiriwa kufikia milioni 106 franka za Burundi sawa na Euro elfu 49 radio hiyo ilizinduliwa mwishoni mwa juma lililopita.

Kupitia mandao wa kijamii wa Twetter fuko la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA ambalo limekuwa likifanya kazi hasa katika kukuza uelewa wa mpango wa uzazi na kwamba radio ni njia ya kuhamasisha wananchi hususan wa viijijini.

Mwenyekiti wa shirika linalofuatilia mwenendo wa wanahabari nchini Burundi Muhozi Innocent anaona ufadhili huo kuwa kashfa kubwa. “ tunashuhudia leo taasisi ya Umoja wa Mataifa inafadhili kituo cha propanganda za rais na mkewe, radio inayomilikiwa na mtu ambaye alivunja vyombo huru vya habari, ameharibu mfumo mzima pamoja na mashjirika huru ya kiraia, anaeshikilia vijana zaidi ya 8000 ambao walioandamana dhidi ya kupinga muhula wa tatu,”.

“Nawakumbusha kwamba mahakama ya kimataifa leo inafahamu ukiukwaji wa haki za binadamu unatekelezwa nchini Burundi. Wasitwambvie kuhusu faida za wasiojiweza.,"

"Kila siku wanatengeneza wasiojiweza kutokana na sera yao mbovu. Kuona taasisi ya Umoja wa Mataifa inatekeleza hilo, ni kinyume kabisa na jukumu lake kuwafadhili washukiwa wa mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.”

Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wananchi halijazungumza lolote kuhusu hilo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.