Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Colombia: Idadi ya waliouawa katika shambulio la Bomu Bogota yaongezeka hadi 21
E.A.C

IGAD yazionya pande zinazohasiamiana Sudan Kusini

media Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini yanasuasua. Hawa hapa ni wajumbe kutoa pande zinazohasimiana nchini humo. AFP PHOTO / Solan Gemechu

Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini huenda yasifike popote baada ya taarifa kuwa utawala wa Juba unatishia kususia mazungumzo haya moja kwa moja ukitaka uwakilishi zaidi kwenye mazungumzo hayo.

Kutokana na madai hayo viongozi wa IGAD waliwajia juu viongozi wa pande zinazohasimiana kuhusu hatua zozote za kutaka kukwamisha mazungumzo ya safari hii na kutishia kuchukua vikwazo dhidi yao.

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Workineh Gebeyehu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mazungumzo hayo, amezilaumu pande hizo kwa kutaka kukwamisha mazungumzo hayo kwa makusudi na kuapa safari hi jumuiya yao itachukua hatua kali dhidi yao.

Tayari nchi ya Marekani imeonesha kuchukizwa na namna utawala wa Juba unavyoshiriki kwenye mazungumzo haya na kuonya kuchukua hatua zaidi dhidi ya viongozi wake.

Machafuko nchini Sudan Kusini yamesababisha vifo vya watu wengi na wengine wengi kulazimika kuyahama makazi yao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana