Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-KATIBA

Wanaharakati 42 wakamatwa nchini Burundi kwa kupinga mabadiliko ya Katiba

Wabunge wa upinzani nchini Burundi wanasema wanaharakati 42 wamekamatwa na kuziwa na maafisa wa usalama baada ya kutangaza wazi wanapinga mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza AFP PHOTO / MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Pierre-Celestin Ndikumana, kiongozi wa shirika la raia linalofahamika kama Amizero y'Abarundi, amethibitisha kukamatwa kwa wanaharakati hao mwezi Desemba mwaka uliopita.

Ndikumana ameongeza kuwa, wanaharakati hao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wafuasi wa shirika hilo lakini pia walionesha msimamo wao kuhusu mchakato huo.

Serikali ya Bujumbura, imekuwa ikionya kuwachukulia hatua wale inayosema watakaobainika kuwapotosha wananchi kuhusu mabadiliko hayo ya katiba ambayo yanapingwa pia na wanasiasa wa upinzani.

Mwezi Desemba mwaka 2017, serikali nchini Burundi ilianza kampeni ya kuwahamasisha raia wa Burundi kukubali mabadiliko ya katiba ili kuongeza muda wa rais kukaa madarakani kutoka miaka mitano hadi miaka saba.

Rais Nkurunziza anaweza kuwania tena urais nchini humo mwaka 2021 na hivyo kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Mzozo wa kisiasa nchini Burundi ulianza mwaka 2015, baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu kinyume na katibana kusababisha jaribio la mapinduzi ya kijeshi.

Takwimu kutoka Mashirika mbalimbali zinaonesha kuwa kati ya watu 500 na 2000 wameuuwa tangu kuzuka kwa mzozo huo, huku wanasiasa wa upinzani wakimbilia nchi za nje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.