Pata taarifa kuu
KENYA-UKEKETAJI

Daktari nchini Kenya akwenda Mahakamani kutaka ukeketaji kuruhusiwa

Daktari mmoja nchini Kenya amekwenda Mahakamani mjini Machakos kutaka kuhalalishwa kwa ukeketaji wa wanawake miongoni mwa jamii zinazotekeleza utamaduni huo.

Maandamano ya kupinga ukeketaji nchini Kenya
Maandamano ya kupinga ukeketaji nchini Kenya pbs.twimg.com
Matangazo ya kibiashara

Ukeketaji ni marufuku nchini Kenya, na yeyote anayekamatwa akijihusisha hufungwa jela miaka mitatu au kutozwa faini ya Dola za Marekani 2,000.

Wanaharakati wanaopinga ukeketaji wanasema kuwa zoezi hilo, limeendelea kukiuka haki za wanawake na kuwaletea madhara ya kisaikolojia.

Hata hivyo, Daktari Tatu Kamau anasema kuwa, sheria hiyo inakiuka haki za kitamaduni za wanawake katika jamii zinazotekeleza ukeketaji kwa lengo la kudumisha mila zao.

Aidha, amesema haijawahi kuthibitishwa kuwa kuwepo kwa madhara yoyote ya kiafya kutokana na zoezi hilo na hivyo kuwabagua wanawake.

Mahakama itasikiliza ombi  hilo mwezi Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.