Pata taarifa kuu
KENYA-UCHUMI

Kenya Airways kuanza safari zake kwenda Marekani

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, linatarajiwa kuanza safari zake za moja kwa moja kwenda Marekani mwezi Oktoba mwaka huu.

Kituo nambari 1 cha uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi, Kenya (2017).
Kituo nambari 1 cha uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi, Kenya (2017). CC BY-SA 4.0/Salama jamaa
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi Januari 11, Kenya Airways ilianza kuuza tiketi kwa ajili ya uzinduzi wa safari zake kati ya Nairobi na New York. Shirika hilo linapanga kufanya safari ya kwanza Oktoba 28, 2018.

Wiki iliyoipita Waziri wa uchukuzi wa Kenya James Macharia alisema wanasubiri jibu kutoka kwa idara ya usafiri ya Makrekani kuhusu ushirikiano husika.

Idara hiyo inatarajiwa kufanya ukaguzi wake wa mwisho wa uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwezi Oktoba kabla ya kuanza kwa safari hizo.

Mwezi uliopita mamlaka ya uchukuzi wa anga ilikuwa imetengaza kwamba ukaguzi wa mwisho uliahirisha mpaka baada ya uchaguzi mkuu.

Wakenya na wasafiri wengine wataweza kununua tiketi zao mapema kwa bei ya Dola za Kimarekani 869, na kuwa tiketi hizo kwa bei hiyo poa ni chache na bei zitaongezeka kadiri watu watavyoendelea kufanya manunuzi.

Hatua itaifanya Kenya Airways kuwa shirika la kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa na safari za moja kwa moja hadi Marekani.

Ndege za shirika hilo zitakuwa zinafasiri moja kwa moja hadi uwanja wa ndege wa JFK, New York.

Kenya Airways itafanikisha safari hizo kwa ushirikiano na shirika la Delta Airlines la Marekani.

Safari hiyo itachukua saa 15 kutoka New York hadi Nairobi na saa 14 kutoka Nairobi hadi New York.

Shirika hilo limesema litatumia marubani wanne na wahudumu 12 wa ndege.

Kenya Airways imesema itatumia ndege zake za kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner ambazo huwabeba abiria 234.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa KQ Michael Joseph uzinduzi huo ni hatua muhimu kwa shirika hilo ambayo imefatia mipango mipya ya kifedha iliyotekelezwa na shirika hilo, akiongeza kuwa safari hiyo italiwezesha shirika hilo kuimarika na kuendelea kuingiza faida.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kenya Airways Sebastian Mikosz alisema safari hizo zitakuwa na manufaa makubwa kwa shirika hilo na kuimarisha ukuaji wa biashara yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.