Pata taarifa kuu
KENYA-EU-UCHAGUZI-SIASA

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wakosoa uchaguzi wa Kenya

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya, walioshuhudia Uchaguzi Mkuu nchini Kenya mwezi Agosti na Oktoba mwaka uliopita, katika ripoti yao ya mwisho wamesema, Uchaguzi huo ulitawaliwa na rushwa, matumizi ya rasilimali za umma hasa kwa viongozi wa chama tawala Jubilee.

Viongozi wa waangalizi wa Uchaguzi nchini Kenya kutoka Umoja wa Uaya
Viongozi wa waangalizi wa Uchaguzi nchini Kenya kutoka Umoja wa Uaya eeas.europa.eu
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa waangalizi hao Marietje Schaake amesema wamelazimika kutoa ripoti hiyo wakiwa jijini Brussels nchini Ubelgiji, kwa sababu serikali jijini Nairobi imekataa kuwakaribisha na kukubali ripoti hiyo.

Aidha, ripoti hiyo imeeleza kuwa, wanasiasa walitumia fedha kuwalipa wapiga kura kuhudhuria mikutano ya kisiasa lakini pia kuitisha Tume ya Uchaguzi, na hivyo kusababisha wapiga kura kutopata uhuru wa kufanya uamuzi.

Mapema wiki hii balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec aliutaka muungano wa upinzani NASA kuwa tayari kulegeza masharti ya madai yao na kuwa na mazungumzo na rais Uhuru Kenyatta.

Kauli hii ilikuja baada ya kiongozi wa muungano wa upinzani (NASA), Raila Odinga kusem akuwa yuko tayari kuapishwa kama rais wa watu.

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga yeye na kinara mwenzake Kalonzo Musyoka wataapishwa mwisho wa mwezi huu, kama rais na naibu raia wa watu.

Wafuasi wao wamekuwa wakisema wanasubiri siku hiyo, huku wafuasi wa rais Uhuru Kenyatta wakihofia kuwa hatua hiyo itayumbisha uchumi lakini pia kuzua mzozo mpya wa kisiasa.

Viongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA wametangaza kampeni ya kitaifa kuhamasisha wafuasi wao kujitokeza kwenye sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga na naibu wake Kalonzo Musyoka tarehe 30 ya Mwezi huu.

Vinara hao wawili wamesema sasa tarehe imeshaafikiwa na kwamba hawatashinikizwa na wafuasi wao kuapa na badala yake wataapishwa kwa kufuata maelekezo ya washauri wao.

Akihutubia kwenye mkutano wa baraza la wananchi mjini Kakamega, Raila Odinga alisema kula kwao kiapo hakuna uhusiano na wao kuwa na uchu wa madaraka lakini wanatimiza wajibu.

Tayari rais Uhuru Kenyatta ametangaza kutowavumulia wanasiasa ambao watajaribu kutatiza usalama wa nchi hiyo na kukiuka katiba ya nchi, akisisitiza kuwa tayari kwa mazungumzo yenye tija lakini sio ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.