Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Kenyatta na Ruto wakanusha madai kuhusu tofauti kati yao

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto wamesema kuwa, hawana tofauti zozote kuhusu uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto wakiwa na kibali kinachothibitisha ushindi wao baada ya matokeo ya uchaguzi yalitangazwa na Tume ya Uchaguzi Nairobi tarehe 11 Agosti 2017, siku chache kabla ya kufutwa na mahakama Kuu.
Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto wakiwa na kibali kinachothibitisha ushindi wao baada ya matokeo ya uchaguzi yalitangazwa na Tume ya Uchaguzi Nairobi tarehe 11 Agosti 2017, siku chache kabla ya kufutwa na mahakama Kuu. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na mashaka iwapo viongozi hao wamekubaliana kuhusu majina yaliyopendekezwa wiki iliyopita na rais Kenyatta, baada ya Ruto kutoonekana wakati wa kutajwa kwa Mawaziri wapya.

Ruto amesema hawezi, kuingilia uamuzi wa rais Kenyatta kuhusu uteuzi wa baraza lake la Mawaziri.

Pamoja na hilo, wawili hao hawajaonesha nia ya kuzungumza na viongozi wa muungano wa upinzani NASA, ambao wamesema mazungumzo ya kisiasa yasipokuwepo, Raila Odinga ataapishwa kama rais wa watu tarehe 30 mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.