Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Raila Odinga: Niko tayari kuapishwa Januari 30

media Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga, Novemba 28, 2017. REUTERS/Baz Ratner

Viongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA wametangaza kampeni ya kitaifa kuhamasisha wafuasi wao kujitokeza kwenye sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga na naibu wake Kalonzo Musyoka tarehe 30 ya Mwezi huu.

Vinara hao wawili wamesema sasa tarehe imeshaafikiwa na kwamba hawatashinikizwa na wafuasi wao kuapa na badala yake wataapishwa kwa kufuata maelekezo ya washauri wao.

Akihutubia kwenye mkutano wa baraza la wananchi mjini Kakamega, Raila Odinga amesema kula kwao kiapo hakuna uhusiano na wao kuwa na uchu wa madaraka lakini wanatimiza wajibu.

Tayari rais Uhuru Kenyatta ametangaza kutowavumulia wanasiasa ambao watajaribu kutatiza usalama wa nchi hiyo na kukiuka katiba ya nchi, akisisitiza kuwa tayari kwa mazungumzo yenye tija lakini sio ya kisiasa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana