Pata taarifa kuu

Wakimbizi wa Rwanda hatarini kutotambuliwa kama wakimbizi rasmi

Mataifa mbalimbali duniani, hayatawatambua tena raia wa Rwanda waliokimbia nchi yao kati ya mwaka 1959 hadi 1988 kama wakimbizi baada ya muda waliopewa kurudi nyumbani kumalizika mwisho wa mwaka 2017.

Wakimbizi 33 wa Rwanda wakisubiri kusafirishwa kwenye uwanja wa ndege wa Kisangani DRC, kuelekea Rwanda.
Wakimbizi 33 wa Rwanda wakisubiri kusafirishwa kwenye uwanja wa ndege wa Kisangani DRC, kuelekea Rwanda. ABDELHAK SENNA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii inaamanisha kuwa, raia hao wa Rwanda hawatatambuliwa kama wakimbizi na hawatapa msaada wowote kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR.

Tehehe ya mwezi Desemba 31 mwaka 2017, ilikubaliwa kati ya serikali ya Rwanda na Shirika la UNHCR pamoja na mataifa mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwapa hifadhi wakimbizi hao kutoka Rwanda.

Mkataba wa kurejesha nyumbani wa wakimbizi uliokubaliwa mwaka 1951, unawataka wakimbizi kurejea katika nchi zao baada ya kubainika kuwa, hawapo tena katika hatari ya kushambuliwa au kunyanyaswa.

Hata hivyo, raia hao wa Rwanda wanaweza kurudi nyumbani lakini, hawatapata msaada wowote kutoka kwa Umoja wa Mataifa.

Wakimbizi wa Rwanda ambao wamekuwa wakiishi katika nchi jirani ya DRC, wamenukuliwa wakisema wanahofia kurudi nyumbani.

Wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi yao ambao wamekuwa wakifahamika kama wakimbizi ni takriban elfu 20 kwa mujibu wa takwimi za Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.