Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Rais wa Uganda aidhinisha sheria ya kuondoa kikomo cha umri wa rais

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada tata uliopitishwa na bunge mwaka uliopita, kuibadilisha Katiba ili kuondoka ukomo wa umri kwa yeyote anayetaka kuwania urais nchini humo.

Yoweri Museveni, rais wa Uganda.
Yoweri Museveni, rais wa Uganda. Capture d'écran al-Jazeera
Matangazo ya kibiashara

Hii inamaanisha kuwa, Museveni mwenye umri wa miaka 73 anaweza kuwania tena urais mwaka 2021, iwapo atachagua kufanya hivyo.

Sheria hii mpya imerejesha mihula ya rais kukaa madarakani, ambapo sasa atahudumu kwa mihula miwili, kila muhula ukiwa na miaka mitano.

Wabunge na Madiwani nao watahudumu kwa miaka saba, kutoka miaka mitano.

Sheria ya awali ilikuwa inamzuia mgombea kuwania urais baada ya kutimiza umri wa miaka 75. Kulingana na sheria hiyo ya awali Yoweri Museveni, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 73 hangeliweza kuwania katika uchaguzi ujao.

Bunge liliidhinishwa mswada huo mnamo tarehe 10 Desemba kwa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge waliohudhuria kikao, wabunge 317 wakiunga mkono na 97 wakapinga.

Hatua ya rais Museveni kuidhinisha mswada huo imekuja wakati ambapo amekuwa akihimizwa na viongozi wa kidini na wanaharakati wa kisiasa kutouidhinisha.

Hata hivyo mswada huo unarejesha takwa la rais kuongoza kwa mihula miwili pekee ya miaka mitano.

Kama rais Museveni atashinda uchaguzi wa 2021 ataongoza nchi ya Uganda hadi 2031.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.