Pata taarifa kuu
UGANDA-RWANDA-UGAIDI

Uganda yawafungulia mashtaka ya ugaidi raia 45 kutoka Rwanda

Uganda imewafungulia mashtaka ya ugaidi raia 45 wa Rwanda waliokamatwa katika mpaka wa nchi hiyo na Tanzania mapema mweiz huu.

Maafisa wa usalama wa Uganda
Maafisa wa usalama wa Uganda ISAAC KASAMANI | AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Polisi Emilian Kayima amesema pamoja na kufunguliwa mashtaka hayo, uchunguzi dhidi yao bado unaendelea.

Wanatuhumiwa kuwa na vitambulisho na nyaraka ghushi. Washukiwa hao hata hivyo, wamesema wao ni Wainjilisti na walikamatwa wakiwa njiani kwenda Tanzania.

Wanazuiwa katika gereza la Nalufenya mjini Jinja.

Rwanda inasema kuwa washukiwa hao ni wanachama wa chama cha upinzani cha Rwanda National Congress ambacho viongozi wake wanaishi nje ya nchi.

Kigali tayari inakiita chama hicho cha kigaidi. Serikali ya rais Kagame imekuwa ikiishtumu Uganda kwa kuendelea kuwapa hifadhi maadui wa Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.