Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Serikali na waasi walaumiana baada ya kuvunjika kwa mkataba wa amani

Serikali ya Sudan Kusini na waasi wamelaumiana baada ya kuvunjika kwa mkataba mpya wa amani, saa chache baada ya kuanza kutekelezwa.

Wanajeshi wa Sudan Kusini
Wanajeshi wa Sudan Kusini REUTERS/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo uliotiwa saini wiki iliyopita jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, ulitarajiwa kumaliza mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea nchini humo kwa miaka minne sasa.

Pande zote mbili zilikuwa zimekubaliana kuanza kutekelezwa kwa mkataba huo kuanzia tarehe 24 mwezi Desemba.

Kiongozi wa waasi Riek Machar amesema vikosi vya serikali vilishambulia wapiganaji wake katika mji wa Yei na Bieh Payam.

“Serikali ya inafanya vitendo ambavyo vinaonesha kuwa, inataka kuendelea kwa vita,” alisema msemaji wa waasi Lam Paul Gabriel.

Naye msemaji wa serikali Lul Ruai Koang amekanusha madai ya kuwashambulia waasi, na badala yake kuwashtumu wapiganaji wa Machar kwa kutekeleza mashambulizi katika maeneo mengine ya nchi hiyo.

Mkataba huo unataka pande zote kuacha mara moja kupigana na kutojihusisha na vitendo ambavyo vinaweza kuleta vita.

Wanasiasa wote walioakamatwa pamoja na wanawake na watoto wanaozuiwa wanastahili kuachiwa huru kwa mujibu wa mkataba huo.

IGAD na mataifa ya Magharibi yameonya kuwa wataokiuka mkataba huo, watachukuliwa hatua kali.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.