Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA

Ufaransa: Majaji wafunga uchunguzi kuhusu kuangushwa kwa ndege ya rais Habyarimana

Majaji wa mahakama ya Ufaransa wanaosikiliza kesi dhidi ya ugaudu wamehitimisha uchunguzi wao kuhusu roketi iliyotumika kudungua ndege iliyomuua rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana na kusababisha mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Rais wa Rwanda, Paul Kagame REUTERS/Eric Vidal
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huu uliochukua muda mrefu ndio ulikuwa chanzo cha kudorora kwa uhusiano kati ya Ufaransa na Rwanda kutokana na tuhuma kuwa wapiganaji wa Kitutsi waliokuwa wanaongozwa na rais wa sasa wa Rwanda Paul Kagame ndio waliohusika katika kuangusha ndege hiyo Aprili 1994.

Roketi hiyo iliangusha ndege ya rais Habyarimana jirani na uwanja wa ndege wa Kigali na kusababisha siku 100 za mauaji yanayodaiwa kufanywa na Watutsi dhidi ya jamii ndogo ya Wahutu aliyokuwa anatoka rais Habyarimana ambapo watu zaidi ya laki 8 waliuawa.

Utawala wa Kigali wenyewe kwa muda sasa umekuwa ukiituhumu Ufaransa kwa kuhusika kuchochea mauaji kwa kuunga mkono utawala wa Kihutu, kuwapa mafunzo wanajeshi na wapiganaji ili kutekeleza mauaji.

Uhusiano ulikuwa shakani tangu mwaka 2014 wakati rais Kagame aliporudia matamshi yake kwa kuwatuhumu wanajeshi wa Ufaransa kuhusika kwenye mauaji hayo.

Uhusiano wa nchi hizi mbili ulizidi kudorora mwezi Octoba mwaka 2016 pale majaji wa mahakama za Ufaransa walipoamua kufungua jalada upya la uchunguzi kuhusu shambulio la ndege ya rais Habyarimana kwa kuwa timu ya raia wa Ufaransa walikuwa miongoni mwa waliokufa.

Mwezi Octoba mwaka huu taarifa kutoka ndani ya uchunguzi huo zilidai kuwa majaji walisikiliza shahidi mpya aliyedai aliona roketi hiyo ikitumiwa kutoka kwenye makao makuu ya wapiganaji wa Kagame.

Ushahidi huu mpya ulishabihiana na ule uliotolewa awali ambao wote unamnyooshea kidole utawala wa Kagame.

Jumla ya watu saba wameshtakiwa katika mahakama za Ufaransa kutokana na mauaji hayo akiwemo waziri wa sasa wa ulinzi wa Rwanda James Kabarebe na Franck Nziza ambaye anadaiwa kuwa ndiye aliyefyatua roketi iliyoangusha ndege.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.