Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Raila Odinga: Niko tayari kwa adhabu ya kifo baada ya kuapishwa

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchin Kenya NASA, Raila Odinga amesema yuko tayari kutumikia adhabu ya kifo baada ya kuapishwa kuwa rais wa watu.

Kiongozi wa Muungano wa Upinzani Kenya, Raila Odinga.
Kiongozi wa Muungano wa Upinzani Kenya, Raila Odinga. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Odinga amesema haogopi adhabu hiyo iwapo ndio itakayoleta haki ya Uchaguzi nchini Kenya.

“Namwambia Mwanasheria Mkuu kuwa tutaapishwa na kufa,” alisema Odinga huku akishangiliwa.

Kiongozi huyo wa NASA, amesisitiza kuwa hakuna kinachomzuia kuapishwa kama rais wa watu, lakini haijafahamika ni lini kuapishwa huko kutafanyika.

Mwanasheria Mkuu wa serikali Githu Muigai, ameonya kuwa iwapo Odinga ataapishwa, atakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, ambayo adhabu yake ni kifo kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo.

Odinga amesema kuwa, hatambui serikali ya rais Uhuru Kenyatta pamoja na Uchaguzi wa mwezi Oktoba, uliompa ushindi.

Marekani imemtaka Odinga kuachana na mipango hiyo na badala yake kuendelea na harakati zake za kisiasa na kupigania haki za binadamu.

Washington DC inataka mazungumzo kati ya Odinga na Kenyatta kutatua mvutano wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.