Pata taarifa kuu
KENYA

Kenya: Mahakama kuu yaagiza Polisi kumlipa msichana wa shule milioni 4 kwa kumdhalilisha

Mahakama kuu ya Kenya imeliagiza jeshi la polisi nchini humo kumlipa fidia ya shilingi milioni 4 za Kenya msichana wa shule ambaye alidhalilishwa kwa kuvuliwa nguo na polisi wakati walipokuwa wakimkagua kama ameficha dawa za kulevya miaka miwili iliyopita.

Baadhi ya wanafunzi wa Kike wanaosoma kwenye shule za nchini Kenya.
Baadhi ya wanafunzi wa Kike wanaosoma kwenye shule za nchini Kenya. http://www.unhcr.org
Matangazo ya kibiashara

Msichana huyo alikuwa miongoni mwa kundi la wanafunzi ambao basi lao lilisimamishwa na polisi kwenye barabara ya Karatina-Nairobi Agosti 5 mwaka 2015.

Kukamatwa kwa basi la wanafunzi hawa kulitokana na polisi kupokea taarifa kutoka kwa wananchi kuwa basi hilo linapiga mziki kwa sauti kubwa huku wanafunzi wake wakionekana kuwa wametumia kilevi.

Jumla ya wanafunzi 45 kutoka shule mbalimbali nchini humo walikuwa wakisafiri kurejea jijini Nairobi wakati wa msimu wa sikukuu.

Kwa mujibu wa watu waliowashuhudia wanafunzi hao walidai kuwa walikuwa wakivuta bangi na hata kufanya ngono ndani ya basi mjini Nyeri.

Wakati polisi walipolisimamisha basi hilo waliendesha msako na kufanikiwa kupata bangi ambayo ilikuwa imefichwa na msichana huyo kwenye nguo yake ya ndani.

Msichana huyo ambaye jina lake linahifadhiwa alipandishwa mahakamani siku inayofuata ambapo alikiri kuificha bangi hiyo na kuhukumiwa kifungo cha nje cha chini ya uangalizi kwa miezi 18.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaliamua kufuatilia sakata la msichana huyo baada ya picha za video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonesha polisi wakimvua nguo msichana huyo walipokuwa wakimkagua.

Katika uamuzi wake jaji John Mativo amesema kuwa upigwaji wa picha na baadae kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa na madhara kwakuwa ziliingilia haki ya usiri ya msichana huyo pamoja na utu wake.

“Nahitimisha kuwa ukaguzi ule ulikuwa kinyume cha sheria na ulikiuka sheria ya haki za mtoto kifungu cha 53 cha katiba, haki ya utu na kutodhalilishwa kwa kuzingatia sheria za kimataifa zinazoongoza jeshi la polisi wakati wanawakagua wanawake.” alisema Jaji Mativo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.