Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, amezindua kampeni ya kuibadilisha Katiba ya nchi hiyo, lenye lengo la kuongeza muda wa rais kukaaa madarakani kutoka miaka mitano hadi miaka saba. Iwapo mabadiliko hayo yatapitishwa, Nkurunziza ana nafasi ya kuwania tena uongozi wa nchi hiyo mwaka 2020 na kuongoza mihula miwili hadi 2034. Hii ni mbinu ya Nkurunziza kuendelea kukaa madarakani ?
Vipindi vingine
-
Raia wa Senegal wamchagua Faye kuwa rais wao mpya
Bassirou Diomaye Faye amechaguliwa kuwa rais mpya wa Senegal.Faye mwenye umri wa miaka 44, mshirika wa karibu wa mwanasiasa mwenye ushawishi Ousamane Sonko, ameahidi kufungua ukura mpya wa uongozi wa nchi hiyo.Kwanini raia wa Senegal wamemchagua Faye ? Tunachambua pamoja na Mali Ali akiwa jijini Paris, na Lutege Musa Lutege akiwa jijini Dar es salaam.27/03/202410:15 -
Makala haya yanatupia jicho uchaguzi wa urais nchini Urusi, nini maana ya ushindi wa rais Vladimir Putin.
20/03/202410:04 -
Burundi: Mgawanyiko kwenye chama kikuu cha upinzani CNL
Nchini Burundi, chama kikuu cha upinzani cha CNL kinashuhudia mgawanyiko baada ya kiongozi wake Agathon Rwasa kuondolewa kwenye nafasi kiongozi wa chama.Hii ilitokea wakati Rwasa akiwa ziarani nchini Kenya.Nini hatima ya kisiasa ya Rwasa ?Tunazungumza naye lakini pia Mali Ali mchambuzi wa siasa za Burundi akiwa jijini Paris.13/03/202410:22 -
Uongozi wa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais Salva Kiir amekuwa ziarani Rwanda na Burundi kuangazia swala la usalama28/02/202410:14 -
Wabunge nchini Tanzania wapitisha mageuzi ya sheria za uchaguzi
Wiki iliyopita, wabunge nchini Tanzania, walipitisha miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao. Tume ya uchaguzi itabadilishwa jina na sasa itafahamika kama Tume huru ya taifa ya Uchaguzi. Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake, watateuliwa na rais baada ya kupokea majina matatu kutoka kwenye Kamati ya usaili.Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kinapinga mabadiliko hayo.07/02/202409:40