Pata taarifa kuu
KENYA-UHURU-USALAMA

Kenyatta: Niko tayari kwa mazungumzo ya kuiendeleza Kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko tayari kwa mazungumzo na viongozi wa kisiasa nchini humo kwa lengo la kuendeleza maendeleo ya nchi hiyo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anasem ayuko tayari kwa mazungumzo kwa minajili ya kuiendelea nchi yake Kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anasem ayuko tayari kwa mazungumzo kwa minajili ya kuiendelea nchi yake Kenya. Reuters/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Rais Kenyatta ametoa kauli hii, wakati akiwahotubia raia wa nchi hiyo katika maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru, yaliyofanayika jijini Nairobi.

Kiongozi wa upinzani NASA, Raila Odinga ambaye kuapishwa kwake kama rais wa wananchi, kuliahirishwa leo, amekuwa akisema kuwa yuko tayari kwa mazungumzo ambayo yatalenga kuwepo kwa Uchaguzi mpya wa urais, lakini Kenyatta amesema hawezi kushiriki katika mazungumzo hayo kwa sababu msimu wa kisiasa umepita.

Raila Odinga ambaye anaendelea kupinga kuchaguliwa kwa rais Kenyatta na Stephen Kalonzo Musyoka, walikua wanatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne Desemba 12 kama rais na makamu wa rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya. Lakini Jana Jumatatu muungano huo ulijirudi na kusema shughuli ya kumuapisha kiongozi wao imeahirishwa kwa tarehe nyingine ambayo haikutajwa.

Wajumbe kutoka nchi za magharibi na Kanisa wanapendelea mazungumzo kati ya rais Kenyatta na Odinga yafanyike kufuatia wasiwasi kuwa njia iliyochaguliwa na upinzani ilikuwa inalenga kuzusha machafuko.

Siku ya Jumamosi rais Kenyatta alisema hayuko tayari kwa mazungumzo yoyote kuhusu mabadiliko ya uchaguzi.

Shinikizo zimekua zikiongezeka kumtaka kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya kuachana na mpango wake wa kuapishwa kama rais wa watu siku ya Jumanne Desemba 12.

Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika tarehe 26 mwezi Oktoba ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.

Uchaguzi huo wa tarehe 26 ulikuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.