Pata taarifa kuu
KENYA-NASA-SIASA

Odinga kutoapishwa siku ya Jumanne kama rais wa Kenya

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umetangaza kusitisha shughuli ya kumuapisha kiongozi wa muungano huo Raila Odinga na kusema kwamba shughuli hiyo imeahirishwa kwa tarehe nyingne ambayo haikutajwa.

Kiongozi mkuu wa muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga,Novemba 28, 2017.
Kiongozi mkuu wa muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga,Novemba 28, 2017. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Raila Odinga ambaye anaendelea kupinga kuchaguliwa kwa rais Kenyatta na Stephen Kalonzo Musyoka, walikua wanatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne Desemba 12 kama rais na makamu wa rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya.

Wajumbe kutoka nchi za magharibi na Kanisa wanapendelea mazungumzo kati ya rais Kenyatta na Odinga yafanyike kufuatia wasiwasi kuwa njia iliyochaguliwa na upinzani ilikuwa inalenga kuzusha machafuko.

Siku ya Jumamosi rais Kenyatta alisema hayuko tayari kwa mazungumzo yoyote kuhusu mabadiliko ya uchaguzi.

Vyombo vya usalama vimejiandaa kuhakikisha haviruhusu mkusanyiko wa upinzani siku ya Jumanne jijini Nairobi wakati rais Uhuru Kenyatta atakuwa akiwaongoza wakenya kuadhimisha siku kuu ya Jamhuri katika uwanja wa Kasarani.

Shinikizo zimekua zikiongezeka kumtaka kiongozi wa muungano wa uypinzani nchini Kenya kuachana na mpango wake wa kuapishwa kama rais wa watu siku ya Jumanne Desemba 12.

Katika taarifa iliyotolewa leo na muungano wa NASA ni kuwa tarehe mpya ya kuapishwa kwa Bw. Odinga na Musyoka, na pia kuzinduliwa kwa mabunge ya wananchi itatangazwa baadaye.

Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika tarehe 26 mwezi Oktoba ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.

Uchaguzi huo wa tarehe 26 ulikuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.