Katika shambulio hilo askari zaidi ya arobaini walijeruhiwa na kwa sasa wanapewa matibabu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Tanzania jini Dar es Salaam, Mnadhimu Mkuu wa jeshi hilo, Luteni Jenerali James Mwakibolwa amesema majeruhi 44 bado wanaendelea vizuri na taratibu za kusafirisha miili hadi Dar es Salaam zinaendelea baina ya serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Amesema miili hiyo inatarajiwa kusafirishwa mapema wiki hii, Jumanne au Jumatano.
Luteni Jenerali Mwakibolwa alisem awalizipokea taarifa za fivo vya askari hao kwa masikitiko, lakini amesem ahawatavunjika moyo wala kutetereka.
Alisema jeshi la Tanzania litasimama imara kwa kutetea na kulinza amani kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa.
Askari wa Tanzania wanaojumuika katika kikosi cha Umoja aw Mataifa walivamiwa na waasi wa Uganda wa ADF Desemba 7 jioni katika eneo moja liliopo kaskazini mashariki mwa mji wa Beni, mashariki mwa DRC.