Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Mwanasheria Mkuu Kenya aonya dhidi ya kuapishwa kwa Raila Odinga

media Raila Odinga anasem ayuko tayari kuapishwa tarehe 12 Desemba 2017. REUTERS/Baz Ratner

Mwanasheria Mkuu nchini Kenya Githu Muigai ameonya kuwa hatua ya kumuapisha rais Raila Odinga kama rais ni ya uhaini. Akizungumza katika afisi za Sheria Bw Muigai alisema iwapo NASA itaendelea na mipango hiyo itakua inakiuka katiba na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya viongozi wa muungano huo wa upinzani.

Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Kenya Githu Muigai ameonya kuwa iwapo kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga ataapishwa wiki ijayo, atafunguliwa mashtaka ya uhaini.

Aidha wanaoendesha shughuli za uundwaji wa mabunge ya wananchi pia wanakiuka Katiba na vilevile watachukuliwa hatua kali, amesema Githu Muigai.

Mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai, alisema alhamisi kwamba ni uhaini wa hali ya juu kwa mtu yeyote kuapishwa kama rais wa nchi hiyo iwapo tayari kuna rais ambaye ameapishwa kwa mujibu wa katiba.

Muigai alikuwa akijibu tetesi kwamba kiongozi wa muungano wa upinzani wa Kenya, Raila Odinga, ataapishwa kama "rais wa wananchi' mnamo tarehe 12 Disemba.

Mwanasheria huyo aliwaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kwamba sheria za uhalifu nchini Kenya ziko bayana kuhusu hatua zinzofaa kuchukuliwa kwa mtu yeyote atakauevunja sheria hiyo

Kauli ya Muigai imekosolewa na Mwanasheria Mkuu wa muungano wa upinzani NASA, Seneta James Orengo ambaye amepuuzilia mbali matamshi hayo na kusema hayana msingi wowote.

Kiongozi wa NASA Raila Odinga, katika hatua nyingine amelaani kile anachosema Marekani imeamua kuegemea upande mmoja katika mzozo wa kisiasa nchini humo, na kuitaka iache kuingilia mambi ya nchi hiyo.

Muungano wa NASA, unatarajiwa kutoa mwelekeo wa shughuli kuelekea wiki ijayo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana