Pata taarifa kuu
TANZANIA

Gazaeti la Mwananchi nchini Tanzania lahofia kutoweka kwa Mwanahabari wake

Uongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited umesema kutoweka kwa mwandishi wake Azory Gwanda tangu Novemba 21 kunauweka rehani uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania.

Wanahabari wa Gazeti la Mwananchi nchini Tanzania  wakionesha picha ya mwanahabari mwenzao Azory Gwanda aliyetoweka mwezi Novemba, wakiwa katika kikao cha wanahabari Desemba 7 2017, jijini Dar es salaam.
Wanahabari wa Gazeti la Mwananchi nchini Tanzania wakionesha picha ya mwanahabari mwenzao Azory Gwanda aliyetoweka mwezi Novemba, wakiwa katika kikao cha wanahabari Desemba 7 2017, jijini Dar es salaam. Fredrick Nwaka ripota wa RFI Kiswahili
Matangazo ya kibiashara

Gwanda ambaye kituyo chake cha kazi kilikuwa Kibiti Mkoani Pwani, Mashariki mwa Tanzania hajaonekana tangu Novemba 21 na inadaiwa alichukuliwa na watu wasiofahamika katika eneo hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo inayochapisha magazeti ya mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti Francis Nanai , amesema kampuni yake imefanya jitihada ikiwemo kulijulisha jeshi la polisi lakini kufikia sasa haijafanikiwa kumpata mwanidhi huyo.

“Tuna wasiwasi kwa sababu kama Azory ametoweka kwa sababu ya kazi yake, inahatarisha uhuru wa waandishi wa habari na kazi zao,”

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga amelitaka jeshi la polisi kuongeza nguvu kumsaka mwandishi huyo na ikiwa ana kosa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Miaka kadhaa iliyopita, Tanzania ilishuhudia matukio ya kuvamiwa na kushambuliwa kwa waandishi wa habari ambapo mwaka 2008 Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwanahalisi Saed kubenea alivamiwa na watu wasiojulikana na kumwagiwa tindikali.

Ripoti yake ripota wa RFI Kiswahili Fredrick Nwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.