Pata taarifa kuu
KENYA-EAC

Raia kutoka mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia Kenya kutumia vitambulisho

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa raia kutoka mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanaweza kuzuru na kufanya kazi nchini humo bila vikwazo vyovyote.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kushoto) akiwa na mgeni wake Rais wa Tanzania, John Magufuli (kulia), 30 October 2016
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kushoto) akiwa na mgeni wake Rais wa Tanzania, John Magufuli (kulia), 30 October 2016 Kenya State House/ Media handouts
Matangazo ya kibiashara

Ametoa kauli hiyo wakati akiwahotubia Wakenya na wageni mashuhuri baada ya kuapishwa kuongoza kwa muhula wa pili na wa mwisho.

Hii inamaana kuwa raia kutoka Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini wanachohitaji ni kitambulisho cha taifa lao na kuzuru Kenya kwa lengo ya kutafuta kazi, kufanya biashara au shughuli nyingine halali.

“Kuanzia leo, mtachukuliwa kama Wakenya. Mtahitaji tu vitambulisho. Mtaweza kufanya kazi kufanya biashara, kufanya kilimo na hata kupata mwezi wa kuoa au kuolewa,” alisema.

“Ninapowakaribisha, nawakumbusha kuwa, sheria zinazowatumiwa dhidi ya wakenya ndizo zitakazitumiwa dhidi yenu,” aliongezea.

Aidha, Kenyatta amesema mafanikio ya Kenya yapo katika mafanikio ya Jumuiya ya ya Afrika Mashariki iliyo thabiti na atashirikiana na marais wenzake kufanikisha hilo.

Mbali na hilo, raia kutoka mataifa yote ya Afrika, watapewa Visa ya kuingia nchini humo katika mipaka ya nchi hiyo kwa lengo la kuhimiza umoja wa Afrika na biashara.

"Leo hii nawaagiza Waafrika wanaopenda kutembelea Kenya, wapewe visa katika mipaka ya nchi, kuonesha hatua ya Kenya kuhimiza umoja wa Afrika,". alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.