Pata taarifa kuu
UGANDA-MGOMO-MADAKTARI

Serikali yaelekea kuelewana na Madaktari wanaogoma

Serikali ya Uganda imeonekana kuwa tayari kutekeleza matakwa ya Madaktari wanaogoma nchini humo na hivyo na kuleta matumaini ya wwahudumu hao kurudi kazini.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni DR
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la kila siku nchini humo la Daily Moniter, limeripoti kuwa kumekuwa na mikutano miwili ya Baraza la Mawaziri na viongozi wa chama cha Madaktari na  mwafaka kufikiwa.

Hata hivyo, chama cha Madaktari nchini humo (UMA) kinasema kinataka makubaliano yoyote kuwekwa kwenye maaandishi ili kuaminiwa zaidi.

“Tunasuburi serikali iyaandike makubaliano haya kabla ya kupiga hatua nyingine,” alisema Daktari Fauz Kavuma msemaji wa chama cha Madaktari.

Madaktari wanataka kulipwa Shilingi za Uganda Milioni 5, kutoka Shilingi Milioni 1.3.

Mbali na nyongeza ya mshahara, Madakatri wanaitaka serikali kutenga fedha zaidi za kununua dawa, kuboresha mazingira ya kufanyika kazi na kuwezesha mafunzo ya mara kwa mara kwa madaktari hao.

Waziri Mkuu Ruhakana Rugunda amekuwa akiongoza mazungumzo haya.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.