Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Mazungumzo mapya kuhusu mgogoro wa kisiasa Burundi kuanza Novemba 27

Mazungumzo mapya kuhusu mgogoro wa kisiasa wa Burundi yanatazamiwa kuanza tena Novemba 27 hadi Desemba 8, kwa mujibu wa timu ya Mwezeshaji katika mgogoro huo, rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Mwezeshaji katika mgogoro wa kisiasa wa Burundi.
Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Mwezeshaji katika mgogoro wa kisiasa wa Burundi. EBRAHIM HAMID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo mapya yatakua ni yenye maamuzi, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na timu ya Mwezeshaji.

Mazungumo haya yatadumu siku 13 ili kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro huo uliibuka baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu wa urais mwaka 2015.

Ajenda ya mazungumzo hayo haijafahamishwa, hata orodha ya watakaoshiriki pia haijafahamishwa. Katika mazungumzo yaliyotangulia, serikali ya Burundi ilikataa kusiriki mazungumzo ya moja kwa moja na upinzani wenye msimamo mkali, ulio uhamishoni (Cnared), ikiushtumu kuhusika katika jaribio la mapinduzi lililotibuliwa Mei 14, 2015. Hata hivyo Mwezeshaji rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa alikua akijaribu kukutana na kila upande katika mgogoro huo.

Wakati huo huo muungano wa vyama vya upinzani ulio uhamishoni, kupitia msemaji wake Pancrace Cimpaye, tayari umetangaza kwamba hautashiriki mazungumzo hayo, ukishtumu Mwezeshaji katika mazungumzo hayo Benjamin Mkapa kuegemea upande wa serikali na kutaka baada ya mazungumzo hayo mazungumzo mengine kuendelea nchini Burundi.

Hivi karibuni kiongozi wa chama tawala CNDD-FDD, Evariste Ndayishimiye, alitembelea Tanzania wiki tatu zilizopita ili kueleweshwa kuwa chama tawala na serikali vinatakiwa kushiriki mazungumzo hayo muhimu.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka balozi mbalimbali mjini Kampala, wanasiasa wa upinzani wanaotafutwa na vyombo vya sheria vya Burundi hawatashiriki mazungumzo hayo.

Mabalozi kutoka nchi mbalimbali za Ulaya na Marekani katika ukanda wa Afrika Mashariki wana wasiwasi na uamuzi huo wa timu ya usuluhishi wa kikanda, ambayo imetenga Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Umoja wa Ulaya katika maandalizi ya mazungumzo hayo ambayo yanaegemea upande wa rais Nkurunziza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.