Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI-HAKI

Hatma ya Kenya mikononi mwa Mahakama Kuu

Tangu Jumatano, Novemba 15, majaji wa Mahakama Kuu ya Kenya wanachunguza rufaa mbili ambazo zinaomba kufutwa kwa uchaguzi mpya wa Rais Uhuru Kenyatta.

Mahakama ya Juu ya Kenya inachunguza kesi za kupinga uchaguzi wa marudio wa rais uliofanyika Oktoba 26, 2017.
Mahakama ya Juu ya Kenya inachunguza kesi za kupinga uchaguzi wa marudio wa rais uliofanyika Oktoba 26, 2017. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Rufaa ya kwanza iliwasilishwa na watetezi wawili wa haki za binadamu, Khalef Khalifa na Njonjo Mue, ya pili na iliwasilishwa Mbunge wa zamani, Harun Mwau.

Katika mjadala huo, kunazungumzia uamuzi wa Raila Odinga kujiondoa katika uchaguzi huo na mvutano na vurugu ziligubika uchaguzi wa Oktoba 26.

"Tume ya uchaguzi haielewi sheria, au inadhani ina uwezo wa kuizuia," anasema mwanasheria Julie Soweto. Walalamikaji wanapinga uchaguzi ambao haukufanyika katika majimbo 25 ya Kenya na mchakato uliogubikwa na machafuko na vitisho, mchakato ambao uliandaliwa na tume chini ya shiniko la utawala.

Walalamikaji wanasema kuwa uchaguzi wa Oktoba 26 ungelipaswa kufutwa kutokana na kujiondoka kwa Raila Odinga. Katika mjadala huo pia, walalamikaji wanataka kupata ufafanuzi wa "uchaguzi mpya", neno ambalo lilitumiwa na Mahakama Kuu Septemba 1.

Kwa wanasheria wa Harun Mwau, mchakato ungelipapaswa kuanza upya tangu mwanzo, na kuteua upya wagombea. "Je, huu ndiyo uchaguzi uliyokuwa unatarajia ya wa kwanza kufutwa? Ikiwa ni pamoja na 38% na 98% ushindi, "anasema mwanasheria akishtumu.

Kwa upande wao watetezi wa IEBC, na hasa ule wa Uhuru Kenyatta, wamewasilisha madai yao wakisema kuwa walalamikaji hawakupiga kura, kwa hivyo hawana haki ya kukosoa mchakato huo, huku wakibaini kwamba madhara ya kijamii na kiuchumi yanaweza kuwa makubwa kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa pili. Mahakama Kuu inatarajia kutoa uamuzi wake siku ya Jumatatu Novemba 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.