Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Raila Odinga: Sitambui matokeo na Uchaguzi "bandia" uliompa ushindi Kenyatta

Siku moja baada ya tume ya uchaguzi nchini Kenya kumtangaza Uhuru Kenyatta kuwa rais mteule, hii leo kinara wa upinzani nchini humo Raila Odinga amejitokeza na kudai kuwa muungano wao hautatambua kamwe matokeo ya uchaguzi aliouta “bandia”, akiapa kufanya maandamano ya amani na kuhamasisha wananchi kutotii Serikali na kuishinikiza kung’oka.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Odinga amesema uchaguzi huu haupaswi kukubaliwa akisema ikiwa watakubali itakuwa ni utani kwa demokrasia na chaguzi na kwamba badala yake nchi yake itaishia kutokuwa na haja ya kupiga kura na viongozi wake kuteuliwa kifalme.

Kauli yake imekuja wakati huu wananchi wengi na hasa wafuasi wa upinzani walikuwa wanasubiri kujua kali ya mwisho ya kiongozi wao kuhusu uchaguzi mkuu wa marudio uliofanyika juma lililopita.

Amesisitiza kuwa, upizani utahakikisha kuwa, Uchaguzi mpya unafanyika kwa mujibu wa Katiba na sheria kama ilivyoagizwa na Mahakama ya Juu.

Kuhusu mazungumzo na rais Uhuru Kenyatta, Odinga amesema kuwa muungano wake upo tayari kwa mazungumzo lakini yawe ni kuhusu maandalizi ya Uchaguzi mpya wa urais.

Aidha, ametangaza Baraza la Wananchi litakalopanga, mikakati mbalimbali ikiwemo kususia uchumi, kuandamana kwa amani na kusimamia sheria.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa tangazo hili la Odinga, linaendelea kuweka pabaya muskabali wa kisiasa nchini Kenya, wakati huu wananchi wakiwa wamegawanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.