Pata taarifa kuu
KENYA-IEBC-UCHAGUZI

Tume ya uchaguzi Kenya kutangaza matokeo ya uchaguzi

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC), inatarajiwa kutangaza matokeo ya Uchaguzi mpya wa urais uliofanyika wiki iliyopita na kususiwa na muungano wa upinzani NASA.

Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi nchini Kenya, Wafula Chebukati.
Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi nchini Kenya, Wafula Chebukati. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutangazwa mshindi kwa zaidi ya asilimia 90, wakati huu kukiwa na maswali mengi kuhusu mkaganyiko wa idadi ndogo ya wapiga kura na matokeo yanayotangazwa.

Tume ya Uchaguzi pia inatarajiwa kutangaza hatima ya majimbo manne Magharibi mwa nchi hiyo, ambayo Uchaguzi haukufanyika.

Kiongozi wa muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga ambaye amesema hatambui uchaguzi huo na kutaka uchaguzi kufanyika, baada ya miezi mitatu, naye anatarajiwa kuwahotubia wafuasi wake leo Jumatatu.

Siku ya Jumapili Odinga alisema uchaguzi huo haikubaliki na kusisitiza kuwa hawezi kustaafu siasa.

Naye Naibu rais William Ruto ameiambia Al Jaazera kuwa, hakuna uchaguzi mwingine utakaofanyika, na mazungumzo na Odinga yatahusu mambo mengine na sio uchaguzi mwingine.

Uchaguzi huu umewagawa Wakenya, huku kazi kubwa ikisalia kuliunganisha taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.