Pata taarifa kuu
BURUNDI-KATIBA-SIASA

Rasimu ya marekebisho ya Katiba yapitishwa Burundi

Nchini Burundi, Baraza la Mawaziri lilipitisha siku ya Jumanne, Oktoba 24, wakati wa mkutano maalum, mapendekezo ya marekebisho ya katiba ambayo yatabadili kwa kina nakala hii muhimu na kuruhusu Rais Pierre Nkurunziza, ikiwa itapitishwa kwa kura ya maoni, kuwania muhula wa nne mwaka 2020.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anaongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu wenye utata.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anaongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu wenye utata. AFP/LANDRY NSHIMIY
Matangazo ya kibiashara

Kwa hili halishangazi wengi nchini humo, ingawa uamuzi huu haujawekwa wazi, kutokana na muda ambao haujapatikana. Muswada huu ulikuwa tayari umeandaliwa tangu zaidi ya miezi sita iliyopita na mazungumzo ya mwisho kati ya Warundi yaliyofanyika bila kuwepo kwa upinzani wenye itikadi kali na vyama vya kiraia. Viongozi wa upinzani kutoka muungano wa CNARED na wanaharakati kutoka vyama vikuu vya kiraia wako uhamishoni tangu kuzuka kwa machafuko nchini Burundi mwaka 2015.

Ibara ya 96 ya Katiba, ambayo inaweka kikomo cha mihula miwili ya miaka 10 kwa rais itaondolewa. Toleo jipya la Katiba ya Burundi inaeleza kuwa rais atachaguliwa kwa miaka saba kama muhula mmoja na kuendelea kama atachaguliwa na wananchi, hata kama hawezi "kuongoza zaidi ya mihula miwili mfululizo."

Hakuna kitu kinachoweza kuzuia Rais Pierre Nkurunziza kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 na kuendelea kusalia mamlakani hadi mwaka 2034, afisa mwandamizi nchini Burundi amesema. Marejeleo yoyote ya makubaliano ya amani ya Arusha yamendolewa kwa ufanisi, kwani ni katazo kwa rais kuongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 10. Kwa mujibu wa afisa huyo mwandamizi, Pierre Nkurunziza anaweza kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2041.

Utawala umejizuia kubadili ibara zinazozungumzia usawa wa kikabila zilizomo katika Katiba ya sasa: 60% ya Wahutu na 40% ya Watutsi katika serikali na bunge, na usawa uliopo katika jeshi na polisi.

Lakini muundo wa serikali utabadilishwa upya: hakuna mfumo wa makamu wawili wa rais. Nafasi zote hizo zitachukuliwa na waziri mkuu kutoka chama kiliopata wabunge wengi na makamu wa rais kutoka upinzani, lakini atakua hana mamlaka.

Kura ya maoni kupigwa mnamo mwezi Februari

Hatimaye sheria rahisi zitapitishwa kwa idadi kubwa inayohitajika bungeni, wakati ambapo hadi sasa ilikua inahitajika theluthi mbili tu. Mpango ambao ulitakiwa kulazimisha chama chenye wabunge wengi kujadiliana na wapinzani wake.

Hakuna tarehe iliyowekwa hadi sasa kwa kura ya maoni ya kikatiba, lakini serikali ya Bujumbura inataka kura hiyo ipigwe haraka. Serikali ya Bujumbura inataka kura ya maoni iwe imepigwa hadi katikati ya mwezi Februari mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.