Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Waangalizi wa Kimataifa wasema hawatatuma waangalizi wao nje ya jiji la Nairobi

Waangalizi wa Kimataifa wanaofuatilia Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika siku ya Alhamisi nchini Ken, wametangaza kutotuma waangalizi wake katika Kaunti mbalimbali nchini humo.

Viongozi wa waangalizi wa Uchaguzi nchini Kenya kutoka Umoja wa Uaya
Viongozi wa waangalizi wa Uchaguzi nchini Kenya kutoka Umoja wa Uaya eeas.europa.eu
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa waangalizi hao kutoka Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya Madola na Taasisi ya Carter, wamesema wamechukua hatua hii kwa sababu za kiusalama.

Hata hivyo, waangalizi hao wamesema watasalia jijini Nairobi kuangalia namna matokeo yatakavyokuwa yanatumwa katika kituo cha kutangazia matokeo.

Hata hvyo, waangalizi wengine kutoka Umoja wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Afrika Mashariki, hawajazungumzia lolote kuhusu wasiwasi wao kuhusu hali ya usalama nchini humo.

Umoja wa Afrika una waangalizi 100, waliotumwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Wito wa waangalizi hao kuhimiza mazungumzo kati ya wanasiasa nchini humo haujafua dafu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.