Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA

Viongozi wawili wa kundi kuu la waasi wa Burundi wakamatwa

Viongozi wawili wa kundi la waasi wa Burundi la FPB, lililobadili jina la Forebu ambalo linajumuisha wanajeshi na polisi ambao walitoroka jeshi la Burundi tangu kuanza kwa mgogoro wa kisiasa nchi humo zaidi ya miaka miwili iliyopita, wameuawa.

Bujumbura, mji mkuu wa Burundi.
Bujumbura, mji mkuu wa Burundi. Wikimedia Commons/SteveRwanda
Matangazo ya kibiashara

Jérémie Ntiranyibagira, mshirika wa zamani wa karibu wa Rais Pierre Nkurunziza ambaye alikua kiongozi tangu kubadilishwa kwa jin ala kundi hili mwishoni mwa Agosti na naibu wake, Kanali Edouard Nshimirimana, walikamatwa siku Jumamosi Oktoba 21 mashariki mwa Tanzania, pamoja na maafisa wawili wa kundi hili.

Taarifa ya kukosekana kwa viongozi wa kundi la FPB zilianza kuonekana kwenye mitandao ya kijamii siku mbili zilizopita. Lakini watu waliowakamata wanahakikisha kuwa walipelekwa Burundi. Msemaji wa kundi hili la waasi Adolphe Manirakiza amehakikisha taarifa hii.

"Jumamosi jioni, karibu saa 3 usiku saa za Afrika ya Kati, tuliwasiliana, anasema Kanali Adolphe Manirakiza. Lakini tangu wakati huo, hatuna taarifa kuhusu viongozi wetu wawili. Taarifa ambazo tunazo ni kwamba walikamatwa na polisi wa Tanzania. Ripoti nyingine zinasema kuwa walikuwa pamoja na askri wa Burundi. "

Polisi ya Tanzania ikihojiwa na RFI-Kiswahili, imehakikisha kwamba haina taarifa yoyote kuhusu watu hawa.

Upande wa Burundi, hakuna taarifa yoyote ispokua ile ya Mshauri Mkuu wa Rais anayehusika na masuala ya Mawasiliano Willy Nyamitwe, ambaye amesema kuwa anajizuia kusema kuhusu kile alichokiita "kundi lililobuniwa ambalo halipo."

Lakini upande wa waasi, wanasema wana ushahidi ambao unaonyesha kwamba Jenerali Jérémie Ntiranyibagira na Kanali Edouard Nshimirimana wanashikiliwa na serikali ya Bujumbura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.