Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UHURU KENYATTA

Uhuru Kenyatta kushinda marudio ya Uchaguzi wa urais bila Raila Odinga

Uhuru Kenyatta anawania urais kwa muhula wa pili. Dalili zote zinaonesha kuwa atashinda Uchaguzi mpya wa urais siku ya Alhamisi.

Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hakikisho hili linakuja kwa sababu, mpinzani wake mkuu Raila Odinga amejiondoa katika Uchaguzi huo kwa kudai kuwa hauwezi kuwa huru na haki.

Kenyatta ni mtoto wa rais wa kwanza wa nchi hiyo, Jomo Kenyatta.

Rais huyo wa sasa mwenye umri wa miaka 55, anatokea kwenye familia tajiri inayomiliki biashara mbalinbali na ardhi nchini humo.

Anawakilisha familia zinazoonekana matajiri nchini Kenya, katika nchi ambayo bado kuna umasikini mkubwa na ukosefu wa kazi.

Alitangazwa mshindi wa Uchaguzi wa mwezi Agosti mwaka 2017 lakini, Mahakama ya Juu ikafuta ushindi wake baada ya kubainika kuwa haikuwa huru na haki.

Kenyatta anatokea katika kabila la Kikuyu lenye idadi kubwa ya watu nchini Kenya, na aliingizwa kwenye siasa na rais wa zamani Daniel Arap Moi mwaka 2002.

Lengo la Moi, lilikuwa ni kwa Kenyatta kumrithi lakini hili halikufanikiwa baada ya kushindwa vibaya katika Uchaguzi huo na Mwai Kibaki aliyekuwa anawakilisha chama cha upinzani NARC.

Baada ya Uchaguzi wa mwaka 2007, uliosababisha machafuko nchini humo na kusabaisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha, Kenyatta aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa fedha katika serikali ya muungano.

Pamoja na hilo, alikuwa miongoni mwa washukiwa wakuu wa watu waliochochea machafuko na kushatakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague.

Mwaka 2014, Mahakama ya ICC ilifuta kesi rais Kenyatta wakati huo akiwa rais baada ya upande wa Mashtaka kusema kuwa haukuwa na ushahidi wa kuendele na kesi hiyo, na kuishutumu serikali kwa kushindwa kutoa ushirikiano.

Kenyatta amekuwa akisema angependa kukumbukwa kama kiongozi aliyebadilisha uchumi wa nchi hiyo lakini pia kwa kuwaunganisha wakenya wengi na umeme.

Mwezi Juni mwaka 2017, alizindua treni ya mwendo kasi kutoka Mombasa hadi jiji kuu la Nairobi, baada ya kumalizika kwa ujenzi wa reli ya kisasa.

Kenyatta analezwa kama mwanasiasa mwenye ushawishi, mwerevu lakini changamoto alikuwa nayo ni mnywaji sana wa pombe kwa mujibu wa siri zilizovuja kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani mwaka 2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.