Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-RAILA ODINGA

Raila Odinga, mwanasiasa asiyechoka kutafuta urais nchini Kenya

Raila Odinga, mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Kenya na Waziri Mkuu wa zamani ameamua kutoshiriki katika Uchaguzi mpya wa urais unaofanyika siku ya Alhamisi,Oktoba 26 mwaka huu.

Raila Odinga, kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA
Raila Odinga, kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Kuna wale wanaosema hatua hii inahitimisha ndoto yake ya kuwa rais wa Kenya baada ya kuwa katika mapambano ya kutafuta uongozi wa nchi hiyo kwa miaka minne ya 1997, 2007, 2013 na ,waka huu wa 2017.

Odinga mwenye umri wa miaka 72, amekuwa kwenye siasa za upinzani nchini humo tangu miaka ya 1980, baada ya kurithi siasa za baba yake Jaramogi Oginga Odinga, aliyekuwa Makamu wa kwanza wa rais nchini humo baada ya nchi hiyo kupata uhuru.

Kiongozi huyo wa muungano wa vyama vya upinzani NASA, amekuwa akisema anataka kukumbukwa kama kiongozi aliyepigania demokrasia, haki na usawa nchini humo.

Odinga alitangaza kutoshiriki katika Uchaguzi huo mpya endapo hakutakuwepo mabadiliko muhimu ndani ya Tume Huru ya Chaguzi na mipaka IEBC baada ya Mahakama ya Juu kufuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta.

Upinzani wake kwa rais Kenyatta umerejesha historia ya baba yake Jaramogi kama ilivyokuwa dhidi ya Jomo Kenyatta, waliokuwa mahasimu wa kisiasa.

Odinga ambaye ni kutoka kabila la Luo, linalopatikana Magharibi mwa nchi hiyo, anafahamika pia kwa kufungwa jela wakati wa uongozi wa rais mstaafu Daniel Arap Moi, katika harakati za kupigania kuwepo kwa vyama vingi nchini humo.

Wafuasi wa Mwanasiasa huyo wamempa majina mengi yanayomfanya kuheshimika kama Baba, Agwambo, Jakom, Tinga na RAO wanasema wanampenda kwa sababu ni mwana mageuzi.

Raila Odinga, anafahamika sana kwa namna anavyowahutubia wafuasi wake katika mikutano ya hadhara akitumia  hadithi, vitendawili, mafumbo na nyimbo.

Wapinzani wake, wanamwita Mzee wa vitendawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.