Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Odinga atoa wito wa kutoandamana siku ya uchaguzi Kenya

media Kiongozi wa muungano wa upinzani Raila Odinga, katika mkutano Nairobi, Oktoba 18, 2017. REUTERS/Baz Ratner

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga, ametangaza Jumanne hii kwamba hajatoa wito kwa maandamano wakati wa uchaguzi wa urais siku ya Alhamisi Oktoba 26.

"Hatuombi watu kufanya maandamano siku ya uchaguzi, wala hatujasema hivyo. tuliomba watu wabaki nyumbani wakati wa uchaguzi," Bw. Odinga alisema katika mahojiano ya BBC, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Takriban watu 2,000 waliandamana Jumanne hii katika mitaa ya Kisumu, mji ulio magharibi mwa Kenya kwenye Ziwa Victoria, wakiitikia wito wa Raila Odinga ambaye ametangaza kususia uchaguzi wa urais wa Alhamisi Oktoba 26.

Bw. Odinga anaamini kwamba uchaguzi huu ambapo anawania Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta hauwezi kuwa huru na wa haki kwa kiasi kwamba Tume ya Uchaguzi IEBC haijafanya marekebisho muhimu.

Serikali na Tume ya Uchaguzi wamesema kuwa zoezi la kupiga kura litafanyika siku ya Alhamisi licha ya maandamano ya kupinga uchaguzi huo yaliyoandaliwa na upinzani.

Uhuru Kenyatta alishinda uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 8 Agosti lakini Mahakama Kuu ya Kenya, katika hukumu yake iliyotoa Septemba 1, ilifuta matokeo ya uchaguzi huo uliogubikwa na kasoro nyingi, kwa mujib wa Mahakama Kuu.

Mahakama iliamuru uchaguzi mpya ufanyike ndani ya siku 60.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana