Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-HISTORIA

Historia ya kisiasa nchini Kenya kufikia mwaka 2017

Kuelekea Uchaguzi mpya wa urais siku ya Alhamisi ni muhimu kufahamu mambo ya kipekee kuhusu nchi ya Kenya.

Bunge la Kenya
Bunge la Kenya kenyan-parliament.
Matangazo ya kibiashara

Kenya ni nchi inayoongoza kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sekta ya utalii ndio sekta inayotoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa hilo.

Nchi hiyo ilipata uhuru wake kutoka kwa Waingereza Desemba 12 mwaka 1963, baada ya mapigano ya muda mrefu kati ya raia wa nchi hiyo ya wapiganaji wa Mau Mau dhidi ya Muingereza kati ya mwaka 1952-1960.

Rais wa kwanza wa taifa hilo alikuwa ni Jomo Kenyatta, baba yake rais wa sasa wa taifa hilo Uhuru Kenyatta.

Kenyatta aliongoza nchi hiyo tangu mwaka 1963 hadi 1978 alipofariki dunia na nafasi yake kuchukuliwa na Makamu wa rais Mzee Daniel Torotich Arap Moi.

Moi baadae alikuwa Rais wa nchi hiyo na kuiongoza kwa muda wa miaka 24 na kuacha madaraka mwaka 2002 baada ya chama tawala cha wakati huo kuondolewa madarakani na chama cha NARC.

NARC ulikuwa ni muungano wa vyama vya upinzani, uliomchagua Mwai Kibaki kuwania urais na kushinda kwa kura nyingi na kuongoza hadi mwaka 2013.

Hata hivyo, mambo yalikuwa mabaya mwaka 2007 baada ya kutokea kwa mapigano ya baada ya Uchaguzi wa mwaka huo na kusababisha vifo vya watu 1,100 na maelfu kukimbia makwao.

Mgombea urais wa wakati huo Raila Odinga kupitia chama cha ODM, alidai kuibiwa kura na rais Mwai Kibaki wa chama cha PNU.

Mvutano huo wa kisiasa ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano na Odinga kupewa nafasi ya Uwaziri Mkuu.

Mwaka 2013, kulikuwa na Uchaguzi mwingine na washindani wakubwa walikuwa ni Uhuru Kenyatta aliyekuwa ameshtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa madai ya kuchochea na kusababisha machafuko ya baada ya Uchaguzi wa mwaka 2007.

Kenyatta alitangazwa mshindi katika Uchaguzi huo, ambao Odinga alidai kuwa aliibiwa kura. Alikwenda katika Mahakama ya Juu kupinga matokeo hayo lakini Mahakama ilitupitilia mbali kesi hiyo.

Uchaguzi mwaka 2017 pia ulikumbwa na utata baada ya rais Kenyatta kutangazwa mshindi na Odinga kupinga matokeo hayo na kurejea tena katika Mahakama ya Juu.

Tarehe 1 mwezi Septemba mwaka 2017, Jaji wa Mahakama ya Juu David Maraga na Majaji wenzake watatu waliamua kuwa Uchaguzi wa urais haukuwa huru na haki na kuagiza Uchaguzi mpya ndani ya siku 60.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.